Taasisi ya Ndoa na Sheria ya Ndoa Tanzania (8)
Maendeleo ya Ndoa  katika uzao wa  Mzee Ibrahimu

Katika makala ya leo, tutaangalia maendeleo ya ndoa yaliyotokana na Mzee wetu wa Imani Ibrahimu kuzaa na mjakazi wao Hajiri na
madhara yaliyotokana na kuzaliwa kwa Ishimaeli. Moja ya madhara ya kupatikana kwa mtoto wa mjakazi ni mgogoro unaoendelea
Mashariki ya Kati, kati ya Waisraeli na Waarabu, wakiwemo Wapalestina.

Katika toleo lililopita  na hili, nilitegemea kuchambua pia mgogoro wa Mashariki ya Kati, chanzo kikiwa ni uvunjifu wa misingi ya Ndoa.
Lakini kabla ya kuangalia mgogoro kati ya Waisraeli na Waarabu na hasa Wapalestina, tutaangalia kwanza hali hiyo kwa mtazamo wa
misingi ya ndoa, kutokana na familia ya  Mzee Ibrahimu kuamua kuzaa na mjakazi wao,  yaani Hajiri.
.
Kwa ufupi, tumeshaona mwendelezo wa misingi ya ndoa tangu kuanzia kwa watu wawili wa kwanza kuumbwa,  yaani Adamu na Hawa.
Na pia tumeona faida na madhara kwa  baadhi ya vizazi  vilivyofuata pale walipovunja    misingi ya ndoa.  Toleo lililopita tuliangalia chanzo
cha matatizo ya baadhi ya mataifa, hasa yale ya Waafrika na Waarabu, ambao kimsingi, yanatokana na laana ya Mzee Nuhu kwa mtoto
wake Hamu. Sikupenda kueleza mengi, kwa sababu ushahidi wa hayo uko wazi.

Hata wewe msomaji unaweza kujiuliza ni kwa nini Waafrika ambao kimazingira tuna rasilimali za  asili nyingi kuliko nchi  za  Magharibi ,
lakini tunaendelea kuwa maskini? Waarabu pamoja na kuishi jangwani, lakini wana mali asili ya mafuta ardhini na bado hawajatengana
na umaskini. Hata mafuta yenyewe wasingeweza kuyachimba bila kutumia akili ya mzungu. Nchi za Afrika , ikiwemo Tanzania,
haziendesheki bila misaada na mikopo kutoka nchi za wazungu na Mashirika yao kama IMF na Benki ya Dunia ( World Bank).
Hii yote ni  kutokana na binadamu kuvunja misingi ya ndoa ambayo  Mungu aliiweka. Waarabu na Waafrika tumekuwa na kila sababu ya
kuendelea  kuishi chini ya laana ya Hamu, ambaye sisi ni matokeo ya uzao wake, kwa sababu ya kuendeleza uvunjifu wa misingi ya ndoa,
ambapo matokeo yake ni kuishi maisha yasiyo tofauti na wanyama ambao hawana akili.

Biblia inamfananisha mtu anayevunja misingi ya ndoa sawa na mtu au kiumbe asiye na akili kabisa. Na kiumbe asiye na akili ni mnyama
au kiumbe mwingine yeyote ambaye sio binadamu.
Tunasoma hivi: “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake (Mithali 6:32).
Mstari huu ni sehemu ya mausia ambayo mama alikuwa anamuusia mwanawe ili ajiepushe na zinaa, kwa sababu zingemwangamiza
nafsi yake.

Waafrika na Waarabu kwa kiasi kikubwa wameendeleza mila na desturi chafu zinazovunja misingi ya ndoa na matokeo yake wamekuwa
kama wanyama, kwa akili zetu kuharibika. Tumepoza akili kwa sababu tumeendelea kuishi maisha yasiyotofautiana na wanyama, kwa
jinsi tunavyoendekeza masuala ya ngono. Isitoshe, hata sheria zetu za nchi zimehalalisha uvunjifu wa misingi ya ndoa, ambapo
mwanaume anaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja  

Mwendelezo huu wa uvunjifu wa misingi ya ndoa  huendelea kuondoa ufahamu wa kawaida wa mwanadamu na kutia upumbavu na
ushahidi wa mambo hayo upo wazi. Gharama ya kuondokana na upumbavu ni kubwa, lakini hatuna budi kuilipa ili tuepukane na laana ya
Hamu, ambaye sisi ni uzao wake. Na njia pekee ya kuepukana na laana hiyo ni kuheshimu misingi ya ndoa kama alivyoiweka Mungu,
ambapo  kila mwanaume anatakiwa kuwa   na mke wake na kila mwanamke anatakiwa kuwa na  mume wake; kama wanataka kuishi
katika kufuata misingi ya ndoa kwa faida yao na kwa vizazi vijavyo.

Hayo yalikuwa ni utangulizi na muhtasari wa makala iliyopita, sasa tunarudi  kwenye mada  yetu ya leo, kuhusu  mwendelezo wa ndoa
katika uzao wa Ibrahimu. Ibrahimu ni uzao wa Shemu katika wale watoto  watatu wa kiume wa Nuhu.Tangu mwanzo tumeona kuwa kile
kizazi ambacho huendeleza uhusiano na Mungu huwa hakijihusishi na uvunjifu wa misingi ya ndoa. Misingi ya ndoa ndio sheria au kanuni
ya kwanza ya Mungu kwa wanadamu.

Historia ya Ibrahimu iko wazi kwa kila mtu. Lakini kitu cha msingi kuhusu  ndoa ambacho tunaweza kujifunza kutoka kwa Ibrahimu ni jinsi
alivyoweza kumheshimu Mungu kwa kuheshimu misingi ya ndoa, hata pale ambapo sababu za kibinadamu za kuvunja misingi ile
zilikuwepo.

Tukumbuke Ibrahimu ndiye aliyekuwa rafiki wa Mungu na siku zote alijitahidi kutii maelekezo yote ya Mungu, hata kama maelekezo hayo
yalimtenganisha na jamaa yake. Lakini kubwa zaidi ni kule Ibrahimu kuweza kuishi na mkewe Sara hadi kufikia umri wa uzee bila kupata
mtoto, hata bila  kumwazia Mungu kwa upumbavu.         Hata baada ya kupata ahadi ya kupata mtoto na ahadi hiyo kuchelewa, bado
waliendelea kumtumaini Mungu kuwa  angeweza kuwapa mtoto wa kurithi.  

Kwa sababu ambazo hata Ibrahimu na mkewe hawakuzijua, ahadi hiyo ilikawia sana kutimia. Kukawia kutimia kwa ahadi hiyo kulimfanya
Sara kuhalalisha mashaka aliyokuwa nayo juu ya ahadi ya Mungu kuwa wangepata mtoto, licha ya umri wao kuwa mkubwa. Hapo ndipo
mke wa Ibrahimu Sara alipoanza kutafsiri upya ahadi hiyo. Tafsiri ailiyopata Sara ni kwamba inawezekana wao kupata mtoto, lakini sio
kutoka kwenye viuno vyao, bali kupitia mjakazi wao Hajiri.

Tunasoma hivi kutoka kwenye Biblia: “Basi Sarai  mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.
Sarai  akamwambia Abramu, basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye.
Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri  mjakazi wake  baada ya kukaa Abramu katika nchi ya
Kanaani miaka 10, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. (Mwanzo 1-6).
Kabla ya Ibrahimu kuruhusiwa na mkewe azae na mjakazi wake, tayari wote wawili walikuwa wanajua kuhusu ile ahadi ambayo Ibrahimu
aliambiwa kuwa angepata mtoto wa kurithi, badala ya Eliezeri aliyekuwa mtumishi  wake. ( Mwanzo 15:3-17). Kwa hiyo hitaji la Ibrahimu la
kutaka kupata mtoto wa kurithi, badala ya mtu mwingine ambaye si mtoto wake lilikuwepo na Mungu alilijua. Mungu alimhakikishia kuwa
angepata mtoto. Lakini ahadi hiyo ilichukua karibu miaka kumi kabla ya kutimia. Kuchelewa kwa ahadi hiyo, ndiko kulikomfanya Sara akate
tamaa ya kusubiri na hivyo akamshawishi mumewe Ibrahimu amchukue mjakazi wao ili apate mtoto wa kurithi.

Kwa upande wa Ibrahimu, tungejiuliza  kwa nini hakukataa kumchukua mjakazi wake? Kwanza ile  ahadi haikufafanua kama Ibrahimu
angepata mtoto lini. Ibrahimu aliambiwa kuwa angepata mtoto kupitia viuno vyake na hii ndiyo iliyowahamasisha kuona kuwa kupata
mtoto kupitia kwa mjakazi inawezekana kuwa ulikuwa ndio mpango aliokusudia Mungu kwani wao tayari walikuwa ni wazee; kwa hiyo
mazingira hayo yalichangia kuwaingiza Ibrahimu na mkewe kwenye mtego huo wa kuzaa na mjakazi.

Ili kuona athari zilizofuata baada ya Ibrahimu kushawishiwa kuzaa na mjakazi Hajiri, tuangalie  Biblia inasemaje: ‘Basi akamwingilia Hajiri,
naye akapata mimba.  Naye (Hajiri) alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake (Sarai) alikuwa duni machoni pake . Sarai  
akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata
mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe. Naye Abramu akamwambia Sara, tazama,
mjakazi wako yu mkononi pako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake, (Mwanzo 16:4-6).

Tumeona kuwa haukuwa mpango wa Mungu Ibrahimu apate mrithi kupitia mjakazi. Madhara ya kwanza kabisa kuanza kuikumba familia
ya Ibrahimu ni wao wenyewe Ibrahimu na mkewe Sarai kuanza kutofautiana na kulaumiana kwa kitendo ambacho wote pamoja
walikubaliana kukifanya. Kwanza kitendo hicho kilivuruga amani ndani ya nyumba yao. Sara alianza kumlaumu mumewe Ibrahimu kuwa
ndio sababu ya yeye (Sara) kudharauliwa na mjakazi Hajiri, na hasa baada ya kupata mimba na Mzee Ibrahimu.

Kimsingi, Sara hakuwa na sababu ya kumlaumu mumewe Ibrahimu kwani ndiye aliyemtaka amchukue Hajiri ili wapate mtoto kupitia yeye.
Kitendo cha Hajiri kupata mimba na  Ibrahimu kulizua mtafaruku, ndani ya familia ya Ibrahimu. Lakini hakikuishia hapo. Hata Hajiri
mwenyewe alijikuta katika mateso ambayo hakuyategemea, kwani alifukuzwa  na Sarai kwa sababu ya kuwa na kiburi mara baada ya
kupata mimba.

Kwa nini Mungu alimkubali Ishmaeli?

Ingawa ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu haikumhusu Ishmaeli, lakini Mungu bado alimpokea Ishmaeli  na kumpa baraka, ingawa baraka
hizo bado  zilitenganishwa na uzao wa Ibrahimu ambao ulitokana na Sara kwa kumzaa Isaka baadaye.

Kwanza Hajiri na mtoto wake hawakuwa na kosa  lolote. Hajiri  siye aliyetaka kupata mimba na Mzee Ibrahimu, bali ni uamuzi wa Sara na
mumewe Ibrahimu ndio waliotaka mtoto kupitia kwa Hajiri. Kwa hiyo, Hajiri aliingizwa katika mpango ambao yeye mwenyewe pamoja na
Mungu hawakuhusika. Ishmaeli naye hakuwa na hatia kwa sababu kuzaliwa kwake, ingawa haukuwa mpango wa Mungu, lakini
alikwishazaliwa na hakuna mtu anayechagua katika kuzaliwa.

Kwa upande wa Ibrahimu na Sara, bado Mungu aliwahurumia kutokana na mazingira ya maisha yao. Kwanza waliishi miaka  mingi ya
uvumilivu na pili ili ahadi ya kupata mtoto ilipochelewa ikawa sababu ya ushawishi kwao kuanza kufikiria vinginevyo. Kama Mungu
asingekuwa amemwahidia Ibrahimu na Sara kuwa wangepata mtoto, basi bila shaka wazo la wao kupata mtoto kupitia mjakazi
lisingekuwepo. Kutokana na mazingira hayo, ndiyo maana leo tuna uzao wa Ibrahimu  uliotokana na Ishmaeli ambao ndio waarabu na
wengine na pia tunao uzao uliotokana na Ibrahimu na Isaka aliyekuja  kuzaliwa baadaye.


Ahadi za Mungu ni kweli na amina

Pamoja na Ibrahimu kupata mtoto, tena wa kiume kupitia Hajiri, bado Mungu hakubadilisha uamuzi wake na ahadi yake ya kuwapa
Ibrahimu na Sara mtoto ambaye alitokana na viuno vyao wawili kama mtu na mkewe. Wakati Ishmaeli anaendelea kukua ndani ya familia
ya Ibrahimu na Sara, Mungu alimtokea tena Ibrahimu na Sara na kuifanya ile ahadi ya kuwapa mtoto kuwa ya kweli.
“Wakamwambia , Yu wapi Sara mkewe? Akawaambia, hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama Sara mkeo atapata mwana
wa kiume,” (Mwanzo 18: 9, 10).

Kwa nini Mungu aliendeleza ahadi yake ya kuwapa Ibrahimu na Sara mtoto wa kiume, wakati tayari walikuwa na Ishmaeli? Kwanza
haukuwa mpango wa Mungu kuwapa mtoto nje ya ndoa yao, kwa sababu kufanya hivyo ingekuwa ni kuvunja misingi ya ndoa aliyoiweka  
Mungu mwenyewe. Mungu hawezi kukiuka Neno lake au kile alichokifanya mwanzoni. Kama Mungu asingekuwa anaheshimu misingi ya
ndoa, basi angemwambia Ibrahimu aoe mke mwingine tangu kipindi ambacho Ibrahimu alikuwa kijana. Lakini Mungu kwa kuonesha
kuwa ile misingi ya ndoa aliyoiweka haikupaswa kuvunjwa kwa sababu  ziwazo zote zile, aliahidi kuwapa mtoto  Ibrahimu na Sara katika
kipindi ambacho kibinadamu walikuwa hawawezi kuzaa.

Kama Mungu angekuwa haheshimu misingi ya ndoa, basi kwake kumwambia Ibrahimu kuoa mke mwingine ingekuwa ni kitu rahisi kuliko
wazee hao kupata mtoto kwa njia ya muujiza – yaani uzeeni.

Hii inatuonesha  kuwa Mungu katu hakubaliani na ndoa ya wake wengi kama ambavyo ilikuja kuwa baadaye  na kisha kuenea mpaka
sasa ikiwa tayari imehalalishwa na dini ya kiislamu kuwa eti Mungu ndiye aliyeruhusu ndoa ya wake wengi kwa mwanaume mmoja.
Kama Mungu angekuwa ameona hitaji la mwanaumme kuwa  na mke zaidi ya mmoja, basi angefanya hivyo kwa Ibrahimu ili apate mke
wa pili kwa hitaji la kupata  mtoto.  Cha ajabu Mungu hakuruhusu hata yule Hajiri awe mke wa Ibrahimu hata baada ya kuzaa naye.   
MAKALA INAYOFUATA YA 9