Taasisi ya Ndoa na Sheria ya Ndoa Tanzania (14)
Ndoa za wake wengi zilitokana na uasi na tamaa za wanaume
TOLEO lililopita tulianza kuangalia maendeleo ya Taasisi ya Ndoa katika mfumo wa Torati (sheria), ulioanza
kutumika katika jamii ya kiyahudi miaka michache baada ya kutoka utumwani nchini Misri. Leo tunaendelea
kuangalia ni kwa jinsi gani Torati iliweza kutumika kudumisha mahusiano ya ndoa katika jamii ya wana wa
Israeli.
Kama tulivyoona katika toleo lililopita kuwa kati ya amri 10 zilizoainishwa na Mungu kwa ajili ya taifa la Israeli, amri tatu
kati ya hizo 10 zilihusu Taasisi ya Ndoa. Sababu kubwa ambayo tunaweza kuipata ya Mungu kuanzisha mfumo wa
sheria, ilikuwa ni kuendeleza uhusiano wake na taifa hilo na kulinda hadhi ya taifa hilo, tofauti na mataifa mengine, kwa
kuhakikisha kuwa misingi ya ndoa ambayo ni kiini cha maendeleo ya binadamu inaendelezwa.
Tukirejea nyuma tunaweza kuona kuwa maisha ya jamii ya kiyahudi nchini Misri kwa zaidi ya miaka 400, ulikuwa
umeathiri kwa kiwango kikubwa utamaduni na uhusiano wao na Mungu aliyeabudiwa na baba zao Ibrahimu, Isaka na
Yakobo. Bila shaka kizazi kipya kilichotokana na familia ya Yakobo kilikosa mwelekeo kuhusu maadili ya dini yao na
hivyo amri hizo mpya zilikuwa na nia ya kuanza kuirejesha jamii hiyo katika mwelekeo mpya wa kumjua Mungu. Kwa
muda wote ambao hao watu waliishi nchini Misri, upo uwezekano mkubwa wa kupoteza utamaduni wao wa kumwabudu
Mungu wa kweli na pia kuacha maadili sahihi yahusuyo misingi ya ndoa.
Kwa nini amri 10 zilitolewa
Hizi amri 10 hazikutolewa bure. Kwa kawaida sheria hutungwa ili kurekebisha mwelekeo mzima wa jamii kutoka upotofu
kuelekea kwenye njia sahihi. Kwa kuangalia mpangilio wa amri hizo 10, tunaweza kubaini kuwa amri hizo 10 zilitolewa ili
kurekebisha jamii ya wana wa Israeli ili kuwapa mwelekeo mpya, tofauti na kule walikotoka na kule walikokuwa
wakielekea. Ni dhahiri kuwa jamii ya Misri kimsingi ambayo ilitokana na mtoto wa Nuhu Hamu, ambaye alilaaniwa na
baba yake, ilikuwa ni jamii ambayo haikuwa na uhusiano wowote na Mungu wa kweli, ukiacha uhusiano wao na miungu.
Wanadamu waliotokana na uzao wa Hamu kama tulivyoona katika makala zilizopita, ziliacha pia misingi ya ndoa.
Mungu kwa kutoa amri 10 pamoja na sheria zingine zilizofuata alikuwa na nia moja tu, nayo ni kuendeleza ahadi yake
kwa Ibrahimu ya kumfanya kuwa taifa ambalo lingeendelea kumjua na kumwabudu yeye kama Mungu wa kweli. Kwa
hiyo amri 10, zililenga kuitofautisha jamii ya uzao wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo na jamii zingine za wanadamu
waliokwisha sambaa duniani, baada ya gharika ziliitokana na watoto wa Nuhu.
Katika mwendelezo wa makala haya, tunakusudia kufuatilia maendeleo ya Taasisi ya Ndoa katika mfumo wa sheria
(torati) ulioanzia na amri 10 na kuendelea mpaka ukomo wake uliotokana na kuanza kwa mfumo wa Agano Jipya.
Aidha, kwa sababu tumeanza kuangalia mfumo wa sheria za Musa, basi uchambuzi wetu utaambatana na kuangalia
pia mchango wa Sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971, katika maendeleo ya Taasisi ya Ndoa.
Hata hivyo, lazima niseme mapema kuwa sitachambua kila kitu kihusucho Taasisi ya Ndoa katika mfumo wa torati, bali
nitakachofanya ni kuangalia mambo makuu mawili ambayo ni ndoa za wake wengi na masuala yahusuyo talaka. Haya
ndiyo masuala ambayo yanatatiza watu wengi na kuonekana kama vile kuna mgongano kati ya Agano la Kale na
Agano Jipya.
Ndoa za wake wengi
Huko nyuma katika mfululizo wa makala haya tulibainisha kuwa mpango wa binadamu kujiingiza katika mfumo wa ndoa
za wake wengi kwa mume mmoja haukutokana na Mungu, bali ni matokeo ya roho ya uasi iliyokuwa inatenda kazi
ndani ya maisha ya mwanadamu walioasi. Kwa kuwakumbusha wasomaji wa makala haya ni kwamba mtu wa kwanza
kuanza ndoa ya wake wengi alikuwa ni Lameki aliyetokana na uzao wa Kaini (Mwanzo 4:16-24).
Tangu kuanzia kwa Kaini watu waliooa mke zaidi ya mmoja, ukiacha Ibrahimu na Yakobo, ambapo sababu za kujiingiza
katika mazingira ya ndoa kama hizo tulizielezea kwa kina katika makala zilizopita, walikuwa ni wale walioacha kwa
makusudi, kufuata mapenzi ya Mungu.
Ingawa Biblia haituelezi kwa bayana maisha ya wana wa Israeli walipokuwa Misri kama walijihusisha na ndoa za wake
wengi au la, lakini tunajua kuwa wale viongozi wao, yaani Musa na Haruni walikuwa ni waume wa mke mmoja. Kwa
kuonesha kuwa Mungu aliheshimu sana misingi ya ndoa, alikataza au kuzuia kuoana kati ya jamii ya kiyahudi na watu
wengine nje ya jamii ya kiyahudi iliyotoka nchini Misri wakielekea kwenye nchi ya ahadi ya Kanaani.
Katazo la kuoa au kuolewa nje ya jamii ya kiyahudi lilisema: “Wale usioane nao; binti yako usimpe mwanawe mume,
wala usimtwalie mwanao mume binti yake. Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume, wala usimtwalie mwanao mume
binti yake. Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakuwakia
hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi” (Kumbu 7:2-8).
Agizo la namna hii lilirudiwa mara kwa mara katika jamii ya kiyahudi. Hata hivyo, katazo hili la kuoana kwa jamii ya
kiyahudi na watu wengine halikuwa na maana ya ubaguzi tu wa kabila au utaifa, bali mantiki yake ilikuwa ni
kuhakikisha jamii inayomjua Mungu wa kweli haichangamani na jamii isiyomjua Mungu wa kweli.
Katazo hili lilikuwa ni kali na adhabu yake ilitisha sana; maana Mungu alisema hasira yake ingewaka juu yao, kama
wangejiingiza katika ndoa mchanganyiko na watu wa mafaifa mengi ya nje ya wana wa Israeli.
Katika ulimwengu wa leo, tatizo si kutokuoana na watu wa kabila nyingine au taifa jingine, bali kinachoangaliwa sasa
ni mfanano wa kiimani. Watu wanaotaka kuoana ni lazima waangalie kwanza imani zao kwa Mungu kabla ya kuanza
kufikiria mambo mengine.
Wako watu waliotamani kuwa kinyume na katazo hilo ambao walipambana na hasira ya Mungu, lakini pia wao
wenyewe walipata hasara. Mfano mzuri ni watu kama mfalme Suleimani, Samsoni aliyemwoa Delila na wengine wengi.
Huko nyuma nilieleza kwa kirefu sababu za kuoa wake wengi na madhara yake.
Sheria yetu ya ndoa
Sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971, inatambua ndoa za aina mbili, yaani ndoa ya mke mmoja au ndoa ya
wake wengi. Sheria hii ambayo ilikuja miaka 10 tu baada ya uhuru, haikuanzisha kitu kipya, bali iliainisha na kutambua
mifumo ya ndoa ambayo tayari ilikuwepo katika jamii za Kiafrika, ikiwepo na Tanzania. Kwa hiyo sheria ya ndoa iliweka
tu utaratibu wa kisheria wa kutambua sio tu aina za ndoa, bali hata taratibu zake zilizokuwa zinatumika katika jamii
kuingiza watu katika Taasisi ya Ndoa.
Hata hivyo, kutambuliwa kwa aina za ndoa na sheria, haina maana kuwa ndoa zote ni sahihi kwa mtazamo wa kiroho.
Ndoa za wake wengi licha ya kuwa hazina mantiki, lakini pia zinamdhalilisha mwanamke utu wake, tofauti na
alivyokusudiwa na Mungu kuwa. Ndoa za wake wengi ni ushahidi wa kutosha kuwa huo ni mkakati wa wanaume
kutimiza tamaa zao mbaya. Ni wale walioshindwa kulinda heshima ya ndoa, ndio waliohalalisha kidini ndoa ya wake
wengi. Lakini kama tulivyoona, wale wote waliojiingiza katika ndoa za wake wengi walifanya hivyo kwa sababu ya tamaa
ya mwili ambayo ni matokeo ya uasi.
Mungu wala Musa hawakuruhusu ndoa ya wake wengi
Wakati dini kama za kiislamu na nyinginezo hudai kuwa ndoa za wake wengi zimeruhusiwa na Mungu tangu Agano la
Kale, lakini hatusomi popote ruhusa kama hiyo kutoka kwenye Biblia. Watu waliooa wake wengi kama mfalme
Suleiman, walikuwa ni waasi kwa sababu waligeuzwa hata mioyo na wake waliowaoa na waliabudu miungu ya wake
zao. Kama tutakavyoona baadaye katika mfululizo wa makala haya ni kwamba, Musa aliruhusu talaka tu na hii ni kwa
sababu ya ugumu wa mioyo ya watu aliokuwa anawaongoza. Bwana Yesu alipoulizwa kuhusu talaka alisema kuwa
Musa alifanya hivyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu wenyewe.
Ndoa za wake wengi ni kinyume na haki za wanawake
Ulimwengu wa kidini na hasa nchi ambazo zinaendeshwa kwa misingi ya kidini zinawanyima haki wanawake kuwa na
uhuru na haki yao ya asili ya kuishi na ndoa ya mume mmoja kama ilivyokuwa mwanzo.Ulimwengu wa sasa
unaotetea Haki za Binadamu, zikiwemo haki za wanawake, umefumbwa kichwani na hofu ya kuibua uchochezi wa
kidini kwa kusema hadharani kuwa ,wanaume kuoa wanawake wengi ni uvunjaji wa haki za binadamu kwa wanawake.
Wanawake nao kwa upande wao huogopa kupinga ndoa za wake wengi kwa hofu ya kupata ‘mashambulizi’ kutoka
kwa jamii ya kiislamu inayoenzi ndoa za wake wengi. Kama wanawake wangeulizwa kama wanapenda ndoa za wake
wengi, bila shaka yoyote wangesema hapana. Kwa sababu kama mwanaume hawezi kukubali kuchangia mke na
mwanaume mwingine, basi kanuni hiyo hiyo ndiyo inayowapa hata wanawake haki ya kutochangia mume na
mwanamke mwingine.
Ndoa za wake wengi ni dalili ya ushenzi na kutokustaarabika
Katika ulimwengu huu, kumekuwepo na vitendo vya kishenzi na kimojawapo ni pamoja na watu kuoa mke zaidi ya
mmoja, Mungu alipowaumba binadamu wawili mume na mke. Binadamu wa kwanza alikuwa na uwezo mkubwa hata wa
kutawala viumbe vyote. Majina ya wanyama na mambo mengi ni ubunifu wa Adamu. Ushenzi tunaouzungumzia ni
matokeo ya dhambi. Dhambi ndiyo mwanzo wa tamaa mbaya ndani ya moyo wa mwanadamu. Ni kutokana na hali hiyo
ya dhambi ndio akili ya mwanadamu polepole ilianza kuwa sawa na mnyama.
Huko nyuma nilieleza kuwa uzao wa wanadamu tulio nao umetokana na watoto watatu wa Nuhu. Ukifuatilia kwa makini
historia ya Biblia, utaona kuwa Waafrika na Waarabu ndiyo jamii ambayo kwa muda mrefu iliendelea kuwa chini ya
kongwa la ushenzi na kutokustaarabika kwa sababu ya laana iliyotokana na babu yao Hamu. Laana hiyo inaweza
kuondoka tu kwa kumwamini Yesu Kristo.
Jamii zingine kama za wazungu hata kama hawamwamini Mungu wa Ibrahimu, lakini hawakujihusisha na ndoa za wake
wengi kwa sababu ya misingi ya uzao wao kutokana aidha na Shemu au Yafethi, watoto wengine wawili wa Nuhu.
Hata hivyo, ilitegemewa kuwa wanadamu wangeweza kustaarabika na kuachana na ndoa za wake wengi, lakini kwa
bahati mbaya dini zilizokuja baadaye zilihalalisha ndoa za wake wengi kutokana na waanzilishi wao kuoa wake wengi
na hivyo kuachana na historia hiyo kwa waumini wao kwa madai kuwa hilo ni Neno la Mungu.
Kama Mungu angependa wanaume waoe wake wengi, isingekuwa shida kuweka wazi katika historia ndefu ya kizazi cha
binadamu.
Jisomee makala ili uelimike na kupanua ufahamu
|