Zijue sababu zinazowafanya Wahindi na Waarabu wang’are kiuchumi
Na Mch. Nathaniel S. Kapela
NDUGU msomaji karibu tena kwenye ukurasa huu ili tuzidi kuichambua jamii ya waasia waliopo nchini kwa lengo la kuona baadhi ya
tabia njema kiuchumi, walizo nazo waasia hawa au baadhi ya hekima wanazozifuata zinazowasaidia kujipatia mali za kujitajirisha kwa
kiwango cha juu sana.

Najua kuwa baadhi ya wasomaji mmeshagundua kuwa ninazungumza mema waliyonayo tu wala sijazungumzia mabaya ni kweli, kwani
lengo hasa ni kuona cha kujifunza si kuchambua tu.

Najua kuwa baadhi ya wasomaji mmeshagundua kuwa ninazungumza mema waliyonayo tu wala sijazungumzia mabaya
ni kweli, kwani lengo hasa ni kuona cha kujifunza si kuchambua tu.

Umuhimu wa kuwa na nidhamu kifedha
Suala la nidhamu ya kifedha na kiuchumi ni mojawapo ya mambo makuu yanayowatenga waasi na wazaliwa wa
wahamiaji wa kiasia labda nianze kulieleza hili kwa mifano.

Nilipokuwa mwanafunzi wa uhandisi nchini India nilibahatika kusoma na kijana mmoja toka familia za kitajiri sana za Tata
na Modi. Ninaposema familia za kitajiri ninamaana ya utajiri ambao hakuna mtanzania ameshawahi kuwanao ni matajiri
hasa.

Familia ya Tata na ndugu zao kina Modi ni familia za ki-parsi wa-parsi ni wahamiaji toka Iran, waliokimbilia India kukwepa
mateso ya wa-Islamu wakati waislamu walipoivamia nchi yao na kuanza kuisilimisha kwa nguvu.

Baadhi ya wa-Parsi hawa walikimbia hadi India, ambako walikubaliwa kuishi India na wafalme wa zamani zile kwa sharti la
kutokueneza dini yao kwa wahindi, ila waliruhusiwa kuolewa na wahindi pamoja kubadili dini za wake na watoto wao.

Wa-parsi hawa waliingia India, utamaduni mpya kabisa ki-uchumi na matokeo  yake ni kuwa matajiri karibu wote
wakubwa nchini India ni wa-parsi, mpendwa msomaji hawa sio matajiri wakuibuka na kuzima kesho, ni matajiri
waliokamata uchumi wa India kwa karne nyingi mfululizo. Ni matajiri ambao walikuwa wamiliki wa mashirika mfano ya
ndege ya India mfumo wa reli n.k kabla hayajataifishwa.

Kuna siku moja katika miaka ya nyuma ambapo J.R.D. Tata mmoja wa viongozi waliopita wa familia ya Tata, alinukuliwa
akimweleza Waziri Mkuu wa kwanza wa India Jawarlal Nehru (m-parsi pia) kuwa “Nipeni uongozi wa shirika la reli la India
(India inaongoza kwa kuwa na mfumo mkubwa kabisa wa reli duniani), ninawaahidi kuwa mkinipa hilo shirika
nitaliendesha kwa faida kiasi cha kuweza kuiendesha Serikali nzima ya India, bila ya kutoza kodi ya aina yeyote toka kwa
raia au mtu awaye yote. Na hivyo kuifanya India kuwa nchi ya kwanza kabisa duniani isiyotoza kodi?” Inasema Nehru
hakufurahia wazo hilo (alikuwa mjamaa) na kumaka”Tata, wewe kila saa unawaza faida tu” hivyo wazo hilo likafa. Lakini
kila mtu anayemfahamu Tata alijua hatanii, kweli angefanya.

Tulipokuwa chuoni hapo nilipata mwanya wa kumchunguza mtoto kwa ukaribu nikagundua kuwa:
(1) Alikuwa mpole mtaratibu na mwenye kuishi vizuri na kila mtu.
(2) Alikuwa mwenye kuvaa nguo za kawaida tu ambazo hata mtu wa kawaida/maskini anaweza kuzimudu.
(3) Alikuwa na bidii na masomo
(4) Alikuwa hanywi, havuti wala hana ukaribu na ma-binti ingawa walikuwa wakijaribu bahati zao kila siku.
(5) Alikuwa kapangishiwa jumba kubwa la ghorofa ambao aliishi yeye na wasaidizi wake tu.
(6)Hakuruhusiwa kujiendesha mwenyewe, aliendeshwa kila alikoenda na alikuwa akiendeshwa na kulindwa na wasaidizi
maalumu wenye uniform, hadi eneo la shule/chuo tu ndipo aliachwa pekee ajichanganye na wengine.

Kilichonishangaza ni ile nidhamu yake, na kila siku tulikuwa tukijiuliza kwa nini wazazi wake hawakumpeleka Marekani
kusoma! Kweli walimpa ulinzi wa kutosha kwani kuna majambazi mno India angeweza kutekwa saa yeyote lakini pia
hakutengwa. Nadhani walitaka azidi kuwa m-parsi wa dhati siyo mmarekani mhindi.

Huyu kijana ni mfano wa namna matajiri wa kweli wanavyolea watoto ili hao watoto watakapokuwa watu wazima wawe na
uwezo wa kushika hatamu za kushikilia utajiri wa mali za familia.

Mambo haya ninayoyazungumza siyo mageni kwa wahindi, wanayaelewa na wanafundishana bayana kila siku, na
wanajua siri au hekima kadhaa za kifedha zinazowafanya washamiri kiuchumi kwa mfano

1. Mhindi akinunua gari ujue ana uwezo wa kununua matatu au zaidi
Nilipokuwa India niligundua tabia kadhaa za wahindi ambazo wamekuja nazo hata huku, ma-profesa wetu wengi walikuwa
wakiendesha scooter tu (pikipiki) wakati karibu wote walikuwa na nyumba za ghorofa na wanasomesha watoto wao
Marekani.

Niliendelea kuwachunguza na kugundua kuwa wahindi halisi wanajua nguvu ya pesa na hawaitumii vibaya na hovyo.
Tofauti na huku kwetu ambapo unakuta kwa mfano mtu ananunua hata gari la mkopo, Mhindi ukimwona ana gari moja
usidhani kuwa ndiyo kipimo cha utajiri wake na kuwa kamimina fedha za zote humo, hapana, ana akiba ya kumtosha.

Mhindi hamimini fedha yako yote ili aonekane na kusifiwa na wenzake kama naye yumo.

2. Wahindi wanaelewa tofauti ya vitega uchumi na vitegua uchumi (asset na liabilities)
Katika mfano uliopita nilizungumza kuwa wahindi siyo watapanyaji ni wawekezaji wa asili tofauti na watanzania wazawa,
wahindi wengi siyo watumbuaji na kamwe siyo watu wa matanuzi kama wenzao, ndiyo wapo wachache watumiaji na
watanuao. Lakini wengi wao ni wawekezaji zaidi, na hii ni kwa sababu jamii yao inataka wawe hivyo.

Bila shaka kila aliyejifunza misingi ya uhasibu anajua kuwa kwenye mizania (balance sheet) huwa kuna upande wa
assets na liabilities, mimi hivi huviita vitega uchumi na vitegua uchumi.

Kwa watu wengi nyumba, gari, shamba, kiwanja n.k vyote ni vitega uchumi, lakini kwa wenye kufahamu hekima hasa za
uchumi si mara zote ya kuwa nyumba, gari, shamba kiwanja ni raslimali au ni kitega uchumi, hivi vinaweza kuwa ni
vitegua uchumi kama haviingizikipato kiwacho chote.

Wahindi wanaelekea kulifahamu hili kuliko wazawa wengi, ukichunguza vizuri wahindi huwa hawakimbilii kujenga nyumba
wakipata hela fulani, badala ya kujenga nyumba au kununua gari zuri la nguvu, wahindi huwekezea fedha zao kwenye
vitega uchumi halisi kama biashara au kazi zitakazowazalishia fedha zaidi.

Wahindi wanaelewa fika kuwa kukimbilia kujenga nyumba au kununua gari mara nyingi kwa mtu wa kawaida ni kujitafutia
kitegua uchumi, badala ya kitega uchumi kwani fedha zako zote zitadumbukia humo.

Mhindi akiamua kujenga nyumba ya kuishi sehemu uwe na hakika kuwa ana mali nyingi tu zinazomwingizia fedha na
kuwa kaamua kufanya mengine ya ziada yasiyo lazima sana kwake.

Siyo kila kitu kinachouzika baadaye na kinachoweza kuwekwa dhamana ni raslimali au kitega uchumi (asset) ni sharti
kiwe na uwezo wa kuingiza kipato.

Wakristo ni lazima tujifunze umuhimu wa hekima za kiuchumi, tujifunze namna ya kutega uchumi kwa akili bila hivyo
tutaendelea kuwa makabwela nchini kwetu wenyewe.

Leo ninaomba ujifunze kitu, kama wewe ni mama au mtoto naomba usikazane kumdai mumeo au mzazi wako kila siku
ajenge nyumba au anunue gari wakati hana vyanzo madhubuti vya uchumi kwa jina la Yesu nakusihi umwambie atafute
vitega uchumi halisi kwanza, si vitegua uchumi, mshauri badala yake aanzishe dispensary, duka la dawa baridi, duka la
rejareja, biashara ya bucha, au kingine chochote vumilia ni vyema muwe wapangaji wenye hela na miradi badala ya
kuishi kwenye nyumba yenu wenyewe ilihali mnalala njaa.

Mwandishi mmoja wa vitabu vya apocrypha, alisema “unapoingia kwenye mji tafuta shamba kwanza, kabla ya kujenga
nyumba”. Cha kushangaza ni kuwa wahindi wanaufahamu usemi huu kuliko wakristo, wakati uko kwenye Biblia zenye
vitabu vya ziada kama zile za Warumi.

Wakristo amkeni, mtafuteni hekima, hekima atawainueni na kuwatajirisha mno.

Msomaji mpendwa kumbuka sisemi kuwa dini za wahindi na wa-Arabu ni bora au miungu yao ni bora hapana, mie
nazungumzia baadhi ya hekima zao kama jamii zinazowafanya wang’are kiuchumi.

3. Wahindi wengi hawaoi mke sababu ya uzuri/kupenda wanapewa wake na wazazi au jamii zao
Tofauti na kizazi kipya cha waafrika wazawa ambao baada ya kuhamasishwa na tamaduni mamboleo za kizungu huwa
hawataki kabisa wazo la kuchaguliwa mke wa kuoa, wahindi wengi ambao siyo waasi, bado hukubali kuchaguliwa wenzi
wa maisha hili nalo husaidia sana kuendeleza nguvu yao ya uchumi.

Pengine ili hili ulielewe zaidi ninaomba nieleze mambo kadhaa niliyoyaona kwenye ndoa za kihindi katika utafiti wangu.
(a) Mke na mume huwa na umoja na ushirika wa juu sana hakuna siri au kufichana, mara nyingi kama mume ni
mwajiriwa mke ndiye mshika fedha zote, mume hubakia na fungu kidogo tu la kutembelea lakini mke ndiye huratibu
fedha kiasi gani wale, waweke benki n.k. Hili linawezekana tu kama wote wanafanana na wana misingi inayofanana.
Mwafrika/mtazania akijaribu hili atalia muda siyo mrefu maana badala ya kuwekwa fedha benki, kanga, wax, soso
zitanunuliwa.
(b) Jukumu la kukuza watoto huachiwa mama, mume hubakia na jukumu la kutafuta na kuhangaikia fedha tu. Watoto
wakiugua, watoto wanapohitaji tuition n.k hiyo ni kazi ya mama, baba anaendelea na mapambano mengine. Kwa
watanzania weusi hasa waliostarabika utakuta, mke anadai apelekwe kliniki, wapeleke kwa pamoja watoto wao hospitali
n.k ukimwambia mama wewe acha kazi ulee watoto tu, upeleke hospitali, uwafundisha lugha zetu za asili n.k kwa
mwafrika mtakosana, kwa jamii ya wahindi mke hata kama ana PhD atakubali, kwani ndivyo alivyo lelewa.
(c) Kwenye jamii nyingi za kihindi, si ajabu kwa kijana kulipwa mahari na wazazi wa msichana, kwa njia moja au nyingine.

Hili hata mimi lilinishangaza sana, lakini nilipofuatilia kwa ukaribu niligundua kuwa hii siyo mahari kama tunavyoielewa
huku, huu huwa ni mchango wa familia ya binti kwa wawili hao ili waanze maisha mara nyingi mahari hiyo huwa ni mtaji
kwa wanandoa hao wapya. Nadhani ndiyo maana mke huwa anakuwa na usemi kwenye uendeshaji wa familia, kama
haki ya kuwa mtunza hazina wa familia n.k mambo ambayo ni ndoto kwa familia ya kiafrika, ambako mke huja kwenye
familia ya mume bila kuingiza mali au vitega uchumi vipya.

Sasa haya niliyoyasema hapa juu ukiyachunguza vizuri yanaelekeza kuwawezesha wahindi kiuchumi, familia ya mhindi
inaundwa ili kuwawezesha kiuchumi, siyo kumfurahisha mume. Ndiyo maana kwa mhindi uzuri wa mke ni mzuri ndio lakini
anaona mbali, mhindi anaona wazi kabisa, kweli anaweza kupata mke mzuri mno lakini akaishia kuwa maskini maisha
yake yote. Kwa kujua hili mhindi anakataa furaha ya muda ili apate kitu cha kudumu zaidi nguvu ya uchumi.

Enyi vijana wa ki-kristo, fungukeni macho leo, msikubali kupitwa na wahindi, achaneni na sera za kufukuzia vibinti vizuri,
ili mvioe licha ya kuwa havina maadili wa nidhamu ya kutosha ki-uchumi au kimalezi ya familia, enyi vijana ni afadhali
kuona msichana “poly” yaani asiye na sura nzuri, lakini mwenye hekima ki-maisha na kifedha kwani hapo ndipo utakuwa
umejipatia mke mwema.


Enyi wakristo amkeni, elevukeni, uchumi wa nchi hii unatwaliwa na waasia kwa sababu, wamejiwekea misingi na
kujijengea hekima inayowatajirisha siyo kwa sababu miungu yao ina nguvu kuliko wetu, sisi tu maduni kwa sababu
temempuuza hekima.

Biblia inazungumza ikimkariri hekima alisema: “…kwa msaada wangu wafalme humiliki, na wakuu wanahukumu haki, kwa
msaada wangu wakuu hutawala, na waungwana na naam, waamuzi wote wa dunia.

Nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona, utajiri na heshima ziko kwangu na utajiri udumuo
na haki pia.

Matunda yangu hupita dhahabu, naam dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natambea katika njia ya
haki katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendea. Tena nipate kuzijaze hazina zao (Mithali 8:15-21)

Enyi wakristo saa imefika, ya kuinua hekima ya kiungu, ili tuizidi hekima ya kihindi, ili tuwazidi ki-uchumi na kujikomboa
na mikatale ya utumwa wa ki-uchumi.
Rudi Ukurasa wa MSEMAKWELI