Pata habari makini kupitia kitengo cha Habari cha WAPO Media
|
Tumia vyombo vyako vya WAPO Radio na MSEMAKWELI kupata maarifa
Kanisa Katoliki lakiri Upentekoste ni
tishio kubwa la karne kwake
Wakati upentekoste unafikisha karne moja hivi sasa tangu wimbi lake lilipoibuka mwaka 1906,
Kanisa Katoliki limekiri kuwa umekuwa tishio, kutokana na imani ya kipentekoste kuingia kwa
kasi ndani ya Kanisa hilo. Imani ya Kipentekoste ndani ya Kanisa hilo inafahamika kama
vuguvugu la ‘Karismatiki’ au maarufu kama Charismatic Renewal Movement. Hayo yalisemwa
na Msaidizi wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, Papa Benedict XVI, Monsinyori Juan
Usma Gomez, ambaye alitoa kauli ya Kanisa Katoliki kukiri kitisho kinachotokana na kukua
kwa upentekoste, wakati wa mkutano maalumu ulioshirikisha wawakilishi wa madhehebu ya
Kipentekoste na Kanisa Katoliki
Msaidizi wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, Papa Benedict XVI, Monsinyori Juan Usma
Gomez, ndiye aliyetoa kauli ya Kanisa Katoliki kukiri kitisho kinachotokana na kukua kwa
upentekoste, wakati wa mkutano maalumu ulioshirikisha wawakilishi wa madhehebu ya
Kipentekoste na Kanisa Katoliki.
Kikao hicho kilichofanyika hivi karibuni Jijini Rome, nchini Italia, kiliandaliwa na Idara ya Kanisa
Katoliki inayoshughulikia masuala ya mahusiano ya makanisa, inayofahamika kama Rome Pro
Unione Ecumenical Center.
Wawakilishi wa madhehebu ya Kipentekoste waliohudhuria mkutano huo ni Bw. Stanley Burgess
kutoka chuo kikuu cha Virginia, nchini Marekani na Ruth Burgess wa chuo kikuu cha Missouri,
nchini Marekani.
Wawakilishi hao walilitaka Kanisa Katoliki kuungana nao ili waumini wake wapate uzoefu wa
kushukiwa na nguvu za Roho Mtakatifu.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Msaidizi wa Papa Monsinyori Gomez,
alilitaka Kanisa Katoliki kutoogopa ukuaji wa imani ya Kipentekoste nje na ndani yake.
“Hakuna ulazima wa kukabiliana na imani ya Kipentekoste kwa uadui, hata kama makundi yenye
mwelekeo wa kipentekoste ndani ya Kanisa yanaonesha uadui wakati mwingine”, alisisitiza
Monsinyori huyo, ambaye pia ni Mshauri wa karibu wa Papa.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mkutano huo, wimbi la uamsho wa Kipentekoste lililoibuka
mwaka 1906 Jimboni Los Angeles, Marekani, limesababisha kuwepo kwa waumini wa
Kipentekoste milioni 600 ulimwenguni kote.
Kikao hicho kimebainisha kuwa hivi sasa imani ya Kanisa Katoliki imeathiriwa na imani ya
Kipentekoste inayotokana na wimbi la uamsho uliopo ndani yake, maarufu kama Charismatic
Renewal Movement.
Moja ya imani za mafundisho ya kipentekoste inayopenya ndani ya Ukatoliki imetajwa kuwa ni
ubatizo wa Roho mtakatifu unaodhihirishwa kwa njia mbalimbali, mojawapo muhimu ikiwa suala
la kunena kwa lugha.
Akizungumzia juu ya kufanyika kwa mkutano huo kati ya Wawakilishi wa Kanisa Katoliki na
madhehebu ya Kipentekoste, Father Bruce William wa Chuo Kikuu cha Saint Thomas, Jijini Roma,
alisema suala la mahusiano ya makanisa ni vyema lifanyike kwa marithiano ya pande husika.
Wajumbe wa mkutano huo wa aina yake walikubaliana kufanya mikutano mara kwa mara, kati ya
makanisa ya Kipentekoste na Katoliki.
Maombi yabadilisha
historia ya maisha
katika familia Dar
Afisa Elimu taaluma wa Wilaya ya Kisarawe,
mkoani Pwani, Bi. Zipora Adriani, mkazi wa
Ukonga, Jijini Dar es Salaam, ameelezea jinsi
familia yake ilivyoponywa na magonjwa
mbalimbali baada ya kuombewa kwenye kituo
cha maombezi, BCIC, huko Mbezi Beach.
Akiongea na Safu ya Shuhuda, mama huyo
alisema yeye pamoja na mume wake na watoto
wake watatu, aliowataja kwa majina ya Benedict
(13), Lucy (10) na Clara (6), walikuwa
wakisumbuliwa na magonjwa kwa muda mrefu
lakini sasa wamepona.
Kuhusu yeye binafsi alisema alianza kuugua
akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu, akichukua
digrii yake ya Elimu, ndipo alipoanza kupata
maumivu makali ya kichwa ambayo
yalimsababishia kuumwa macho na kupoteza
uwezo wa kawaida wa kuona.
Aidha, alisema hali hiyo ilimlazimu kusimama
masoma kutokana na kuugua mara kwa mara
na muda wote alikuwa akikaa nyumbani na
kwenda hospitali ya Hindu mandali alipokuwa
akipata matibabu.
“Baada ya kwenda hospitali, vipimo vikaonesha
kwamba nina sumbuliwa na ugonjwa wa moyo,
wakanipa dawa za kutumia lakini hali
haikubadilika nilizidi kuumwa na hali ikawa
mbaya sana”, alisema Afisa huyo.
Akiwaelezea watoto wake alisema walikuwa
wakisumbuliwa na ugonjwa wa pumu tangia
wakiwa wadogo (miezi sita), hali ambayo
iliwafanya kuugua ugonjwa wa mafua na
kubanwa na kifua kwa muda wote.
“Kwa miaka yote watoto wangu walikuwa
wagonjwa wa pumu lakini tangu wameombewa
hapa ni muda mrefu hawaugui tena kifua wala
mafua na pumu wamepona”, aliongeza kusema
mama huyo.
Safari yake ya kuelekea muujiza wa uponyaji
kwake na familia yake ilianza baada ya kusikia
tangazo la ibada za maombezi kwa watu wenye
magonjwa na matatizo sugu kupitia WAPO Radio
Fm, ndipo alipomuhimiza mume wake waende
kwenye kituo cha maombezi na ushauri wa
kibiblia BCIC, Mbezi Beach.
Mama huyo alisema siku ya kwanza
walipokwenda waliombewa na alishangazwa
kutokwa na mapepo ambayo yalijidhihirisha wazi
baada ya kufanyiwa maombi na tangu siku ile
historia ya maisha ya familia yao ikabadilika
kuanzia, baba, mama na watoto wote wakapokea
uponyaji.
“Namshukuru Mungu kwa ajili ya huduma hii,
tangu nilivyoombewa nikaanza kuona kama
kawaida, maumivu ya kichwa yakaisha, nimerudi
chuoni kuendelea na masomo yangu”, alieleza
mama huyo.
Hata hivyo, alisema watoto wake waliokuwa
wakisumbuliwa na pumu nao wamepona na
mume wake alikuwa hana amani sasa ana
amani na wanaishi kwa furaha nyumbani kwao.
Aishi na Jini kama mume wake kwa miaka 15
- Mwenyewe asema haikuwa ridhaa yake
Bi. Rogathe Shao (36), mkazi wa Kimara, Jijini Dar es Salaam ametokwa na mapepo mahaba yaliyokuwa yakimwingilia
kimwili bila ridhaa yake kwa zaidi ya miaka 15, imefahamika. Alisema kabla ya kwenda kuombewa huko BCIC, alikuwa
akienda kwa waganga wa kienyeji ambao walimweleza kwamba alikuwa ametupiwa jini mahaba na mwanamke mmoja
ambaye alisababisha aachane na mume wake. Hali hiyo ilisababisha aachane na mume wake tangu mwaka 1992, baada ya
kuishi naye kwa miaka mingi na kubahatika kuzaa naye mtoto mmoja wa kike aliyemtaja kwa jina Mercy.
Bi. Shao alisema kwa muda wote huo, alikuwa akiingiliwa kimwili nyakati za usiku na mwanaume asiyemfahamu tena
pasipo ridhaa yake, lakini anapostuka na kuamka anajikuta yuko peke yake kitandani hali ambayo ilikuwa ikimwogopesha
sana, ndipo alipoamua kwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta tiba lakini hakufanikiwa mpaka alivyokwenda kwenye kituo
cha BCIC, kuombewa kwa jina la Yesu. “Siku niliyofika kuombewa nikaanguka chini na kupoteza fahamu lakini baadaye
fahamu zikarudi nikaamini majini yaliyokuwa yakinisumbua kwa muda mrefu yamenitoka”, alisema mama huyo.
Aidha, alisema hajatokewa na hali kama ile ya awali tena tangu ameombewa na kuamua kujisalimisha kwa Bwana Yesu,
hivyo, aliwaomba wanawake wenzake wenye matatizo kama hayo kwenda kituoni hapo kwa maombi na ushauri wa Neno la
Mungu ili wawe huru.
MAISHA NI SAFARI YA MILIMA, MABONDE LAKINI NI HALISI (HUU NI USHUHUDA WA HAJABU)
|
WAPO MISSION INTERNATIONAL
|